Header Ads

Breaking News
recent

Mwanamke wa kwanza kutembelea nchi zote 196 ulimwenguni.

Mwanamke huyu wa Marekani ametembelea nchi zote 196 na kuweka rekodi ya dunia
Huenda wewe ni mmoja ya watanzania ambao hajawahi kufika katika kila mkoa hapa Tanzania, kuna mwanamke wa Marekani ambaye amefika kwenye kila nchi duniani. 
Cassie De Pecol
Kama haitoshi, ameweza kufika katika nchi zote 196 ndani ya miezi 18 na siku 26. Cassie De Pecol amevunja rekodi ya Guinness World iliyokuwepo mwanzo.

Mwanamke huyo alianza safari yake July 2015, akipigia debe utalii endelevu kama balozi wa taasisi ya International Institute of Peace Through Tourism.

Jumla, De Pecol ametumia bajeti ya $198,000 kuizunguka dunia. Pia hakuna kitu utakachofanya kisikose kuwa na changamoto, na moja wapo ya changamoto alizopata Cassie ni masuala ya viza za nchi mbalimbali.
 Endapo huenda umeshindwa kutembelea mikoa mbalimbali ya hapa Tanzania, basi chukua time utenge bajeti yako kidogo ili utembelee vivutio vyetu vya hapa Tanzania, vivutio ambavyo wageni wengi duniani wanakuja kuvitembelea kutoka mbali sana na wanatumia gharama kubwa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.