Header Ads

Breaking News
recent

Mozey Radio kuachia Album ya Gospel inayoitwa 'Kilimanjaro'.

Mlima Kilimanjaro unapatikana hapa nyumbani Tanzania, na ni moja kati ya maajabu yanayofahamika duniani kote.

Tumesikia ngoma nyingi sana kutoka kwa wasanii mbali mbali hapa nchini wakiimba kuhusu Kilimanjaro, lakini mambo mawili mapya ninayotaka kukufahamisha wakwetu ni kutoka kwa mmoja wa kundi la Goodlyfe, Mozey Radio kuachia Album ya muziki wa Injili na pili Album hiyo inaitwa "Kilimanjaro"

Album hiyo iliyopewa jina la mlima Kilimanjaro itaachiwa na lable ya Swangz Avenue.

Mozey Radio pia anatamba na hit single yake inayoitwa 'Juicy Juicy'.

Habari kutoka katika mtandao wa Uganda, ni kwamba album hiyo imeandikwa na Radio mwenyewe, huku producer akiwa ni
 Eli Arkhis na Benon.

Radio atabaki kuwa sehemu ya kundi la Goodlyfe pamoja na Weasel japokuwa album hii ni ya Radio mwenyewe.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.