Header Ads

Breaking News
recent

India na rekodi mpya ya kurusha Satelaiti 104.

India imeweka rekodi mpya kwa kuwa taifa lililorusha setilaiti nyingi angani kwa wakati mmoja baada ya kurusha setilaiti 104 kwa pamoja.

Rekodi ya awali iliwekwa na Urusi mwaka 2014, ambayo ilikuwa setilaiti 37.

Kati ya setilaiti hizo zilizorushwa India, ni tatu pekee ambazo ni za taifa hilo. Nyingi ni za Marekani.

Setilaiti hizo zilirushwa kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Sriharikota katika eneo la Andhra Pradesh mashariki mwa India.

Source: BBC Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.