Header Ads

Breaking News
recent

WHO yazihimiza nchi mbalimbali kuchukua tahadhari kuhusu maambukizi ya mafua ya ndege.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO Bibi Margret Chan amezitaka nchi mbalimbali kuchukua tahadhari kuhusu mafua ya ndege, ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo. 

Bibi Chan amesema, tangu mwezi Novemba mwaka jana, takriban nchi na sehemu 40 zimetoa ripoti kuhusu maambukizi ya mafua ya ndege.

 Bibi Chan amesema, mafua ya ndege ya aina ya H5N6 yanayoathiri vibaya bara la Asia, yanatokana na kubadilishana kwa jeni kati ya virusi vya aina 4 za mafua ya ndege.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.