Header Ads

Breaking News
recent

Mtanzania Alphonce Felix Simbu ashinda dhahabu Mumbai Marathon

Tanzania imekua ni nchi moja wapo barani Afrika ambayo imekuwa ikishiriki mchezo wa riadha katika mashindano makubwa kama vile Olympic na mengineyo mengi, japo matokeo huwa si kama wengi ambavyo huwa wanatarajia, japo ushindi huwa upo.

Sasa hii ni moja kati ya stori ambayo kwa sasa imekuwa na msukumo mkubwa kwangu na kwa wanahabari kutaka uijue...

Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu ameibuka mshindi na kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya riadha ya dunia ya Mumbai Marathoni yaliyofanyika nchini India.

Simbu ametumia masaa 2 dakika 9 na sekunde 32, na kuwapiku Joshua Kirkorir wa Kenya aliyeshika nafasi ya pili aliyetumia saa 2, dakika 9 na sekunde 50 na Eliud Barbgetuny wa Kenya alishika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2 dakika 10 na sekunde 39.


Akizungumzia ushindi huo, Simbu amesema siri kubwa ya ushindi wake katika mbio hizo ni mazoezi aliyoyafanya katika milima mbalimbali ya Tanzania, yaliyomfanya awe imara zaidi katika mazingira ya mashindano hayo yalikuwa yanakabiliwa na kona pamoja na vilima vingi.

Jambo lingine lililomsaidia ni uzoefu alioupata katika mashindano mengine ikiwemo Olimpiki za mwaka jana na mashindano ya ubingwa wa dunia ya Beijing mwaka 2015.

Simbu anakumbukwa pia kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika nchini India mwaka jana kwa kukamata nafasi ya tano katika mbio za marathoni.
Source: CRI Kiswahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.