Header Ads

Breaking News
recent

Mike Tyson mkongwe wa masumbwi kumnoa Chris Brown ili amchape Soulja Boy ulingoni.

Kumekuwa na mzozo kati ya wasanii wawili wa Marekani yani Chris Brown pamoja na Soulja Boy kwa takribani muda kadhaa.

Sasa story iliyotoka leo ni kuhusu mkali wa zamani wa masumbwi Mike Tyson amethibitisha kuwa atampa mafunzo Chris Brown kwa pigano lake kufuatia mzozo na mwanamuziki Soulja Boy.

Mwanamasumbwi huyo bingwa wa uzani wa juu aliombwa na mwanamuziki 50 Cent, kufuatia mzozo mbaya kati ya Chris Brown na Soulja Boy wiki chache zilizopita.

Nitamfunza vile atauma sikio la mtu," alisema Mike Tyson.
"Nitamfunza kila mbinu chafu. Kwa sababu siwezi kumfunza jinsi ya kukimbia."
Chris Brown
Soulja Boy anafunzwa na bingwa mwingine wa ndondi, Floyed Mayweather.

Pigano hilo la raundi tatu litafanyiwa huko Las Vegas tarehe ambayo haijatangazwa.
Mzozo huo ulianza pale Soulja Boy aliandika maoni chini ya picha ya Karrueche Tran, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Chris Brown.

Wote hao walinza kuchapisha picha na video za kutishana.
Soulja Boy ndiye aliandika kuhusu pigano hilo lakini akaondoa ujumbe huo badaye.

50 Cent amemuanga mkono Soulja Boy na kusema kuwa atatoa dola laki moja kwa matokeo ya pigano hilo.
Soulja Boy

Chris Brown wa umri wa miaka 27 na Soulja Boy 26, wamekosolewa na wasanii wengine kwa kuzozana hadharani.
Soulja Boy aidha analaumiwa kwa kutumia pigano hilo kama njia ya kufufua taaluma yake ya muziki inayofifia.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.