Header Ads

Breaking News
recent

China Watoto milioni 18.6 wamezaliwa kwa mwaka 2016.

Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini China ilikuwa ya juu zaidi tangu mwaka 2000 licha ya kushuka kwa idadi ya wanawake waliofikisha umri wa kuzaa, kwa mujibu wa maafisa nchini humo.

Kuongezeka huku kumetokana na china kuondoa sheria zake za mtoto mmoja mwaka mmoja uliopita.
Watoto milioni 18.6 walizaliwa mwaka 2016 ambalo ni ongezekeo la asilimia 11.5 kutoka mwaka 2015.

Zaidi ya asilimia 45 ya watoto waliozaliwa mwaka 2016 walikuwa na ndugu mmoja au wawili wakubwa.
Maafisa wanasema kuwa ifikapo mwaka 2020 kati ya watoto milioni 17 na 20 wanatarajiwa kuzaliwa nchini China kila mwaka.

Wanakadiria kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na zaidi ya watu milioni 30 zaidi watakaofanya kazi nchini China.

Sheria za kuzaa mtoto mmoja nchini China zilianza kutumika mwaka 1979 na zinaripotiwa kuchangia China kupoteza watu milioni 5 kila mwaka hali ambayo itashuhudiwa miaka kadhaa inayokuja.

Credit:BBC Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.