Header Ads

Breaking News
recent

Sayansi Na Teknolojia - Ni kwanini mayai yana umbo la duaradufu ambalo sehemu moja ni ndogo kuliko nyingine?

Ukisukuma yai la kuku mezani, haliendi mbele kwa njia inayonyooka, bali linakwenda likigeuka na mwishowe litarudi.

Umbo hilo linasaidia kuyazuia mayai yasipotee. Lakini umbo la mayai ya ndege wa aina mbalimbali lnatofautiana kidogo. 


Ndege wanaojenga viota juu ya jabali huzaa mayai yenye sehemu moja iliyo ndogo zaidi. Mayai hayo yakitoka kwenye viota hayawezi kwenda mbali, na kujizuia kuanguka kutoka jabalini. 

Ndege wanaozaa mayai mengi kwa wakati mmoja pia wanazaa mayai yenye sehemu moja iliyo ndogo zaidi, kwani ni rahisi kwa mayai ya umbo hilo kuwekwa kwa mpango wa mduara, na kupashwa joto kwa uwiano wakati yanapoanguliwa.

Tofauti ya mayai ya ndege, kasa hawana haja ya kuangua mayai yenye umbo la duaradufu. Kwanza, mayai yao yanafunikwa na mchanga na hayapotei. Pili, kasa hawatotoi mayai, hivyo hawana haja ya kuweka mayai katika mduara. Hivyo mayai ya baadhi ya kasa yana umbo la duara.


Lakini baadhi ya mayai ya kasa yana umbo la duaradufu refu, hasa mayai ya kasa wadogo. Mayai yenye umbo la duara yana kipenyo kikubwa zaidi kuliko yale ya duaradufu, hivyo ni vigumu kwa kasa wadogo kuzaa mayai ya duara.


Source: CRI Kiswahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.