Header Ads

Breaking News
recent

Ndege ya Amazon isiyo na rubani (droni) imefanya majaribio ya kwanza ya kusafirisha bidhaa.

Je, iko siku ndege zisizo na rubani (droni) zitaonekana mara kwa mara kama malori? Kampuni ya Amazon imefanyia majaribio ya kwanza ya kusafirisha bidhaa kwa ndege isiyo na rubani (droni) huko Cambridge, Uingereza.

Droni hiyo inaruka bila kuendeshwa na bindamu, na inaweza kupeleka bidhaa kwenda mahali fulani ikiongozwa na GPS. Sasa ndege isiyo na rubani ina uwezo wa kusafirisha bidhaa yenye uzito usiozidi pauni 5. 


Video iliyotolewa na kampuni ya Amazon kwenye tovuti yake inaonesha kuwa ndege isiyo na rubani ilipeleka king'amuzi kidogo kinachounganishwa na mtandao wa Internet na mfuko wa bisi kwenda nyumba ya mteja kwa dakika 13 tu. 


Ndege iliporuka ilikuwa mita 120 kutoka ardhini. Nyumba ya mteja huyu iko karibu na ghala la Amazon, tena ina ua mkubwa unaofaa kutua kwa ndege isiyo na rubani.

Hivi sasa kampuni ya Amazon imetoa huduma hii kwa wateja wawili tu. Inatarajia kutoa huduma hii kwa wateja wengi zaidi wanaoishi karibuni na ghala katika miezi kadhaa ijayo. Lengo la kampuni hiyo ni kufikisha bidhaa katika nyumba za wateja ndani ya nusu saa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.