Header Ads

Breaking News
recent

Msanii Darasa bado anazidi kuwaingia Watanzania na wasio Watanzania.

Darasa ni msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Tanzania anayefanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwa wakati huu. 

Muziki wa hip hop huenda ukawa ni muziki usiopitwa na wakati, lakini huenda ukawa ni muziki wenye mashabiki wa aina yake, ukilinganisha na aina ya muziki wa Bongo Flava unavyo badilika mara kwa mara na kuwakamata mashabiki wengi nje na ndani ya Tanzania.

Lakini msanii Darasa kipindi cha nyuma alikua akiimba aina flani za nyimbo zenye ujumbe kwenye jamii, huenda hazikuwapa hisia watu wengi, hadi hapo alipobadirisha miondoko ya swagger na kuwakamata mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Darasa ni kati ya wasanii waliotoa nyimbo mfululizo na zikapendwa, kwamfano Kama Utanipenda, Too Much, na Muziki alimshirikisha Ben Pol.

Tumeona viedo kibao watu wakicheza wimbo mpya wa Darasa, hadi tukaona Dereva na watu wake wakiingia matatani baada ya kuonekana wakicheza wimbo huo huku akiwa anaendesha gari kinyume na sheria.

Sio hivyo tuu baadhi ya Mastaa wenzake wamekubali kazi zake na kutoa support kazi yake, kama vile Prof. Jay
Kupitia mtandao wa Instagram, ameandika haya:

Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP,
SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS
#ACHA MANENO WEKA MUZIKI
@darassacmg @darassacmg

 Lakini pia Miss Tanzania 2016 Diana Edward ameonyesha uzalendo wa hali ya juu katika kuutambulisha muziki wa kizazi kipya kwa nafasi aliyopata huko alikoenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo wa dunia, ikiwa ni baada ya kuonekana akiwa na Miss Honduras 2016 na Miss Mexico 2016 wakicheza wimbo mpya wa Darasa - Muziki... watazame hapo chini.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.