Header Ads

Breaking News
recent

Maajabu ya mwaka 2016 'Mchele wa plastic!' wagunduliwa.

 Bado kuna matukio ya ajabu bado yanazidi kuikumba hii dunia, watu wamekuwa na njia mbali mbali za udanganyifu, hayo yote ni kwaajili ya kujipatia kipato (ambacho sio halali).

Leo nimekutana na hii stori iliyoripotiwa na mtandao wa BBC Swahili kuhusu kukamatwa kwa mchele wa plastic Nigeria.... endelea hapo chini.

 Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos. 

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo. 

Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice". 

Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".

Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki. 
Source: BBC Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.