Header Ads

Breaking News
recent

Helikopta ya kwanza ya abiria nchini China yenye uwezo wa kubeba tani 7 yaruka kwa mara ya kwanza.

Helikopta ya kwanza ya abiria nchini China imefanya safari yake ya kwanza hii leo, ikiwa ni ishara ya maendeleo mapya katika sekta ya usafiri wa helikopta nchini China.

Shirika la Usafiri wa Anga nchini China limesema, helikopta hiyo AC352 inatumia injini mbili, ina uwezo wa kubeba tani 7.5 wakati wa kupaa, na inaweza kubeba abiria 16.

Mbunifu mkuu wa helikopta hiyo Lu Weijian amesema, helikopta hiyo inaweza kutumika katika usafirishaji wa pwani, uokoaji, utekelezaji sheria, usafiri wa kawaida, na huduma za afya.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.