Header Ads

Breaking News
recent

Shirika la Umoja wa Mataifa lasema huenda mwaka 2016 ukawa na joto zaidi katika historia

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Hali ya Hewa la Umoja wa Mataifa imesema, huenda mwaka 2016 ukawa na joto zaidi katika historia, na hivyo kutahadharisha kuhusu athari mbaya ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Tahadhari hiyo imetolewa wakati wataalam na wapatanishi wa hali ya hewa wakikutana mjini Marrakech, Morocco, kwa mara ya kwanza baada ya kupitishwa na kuanza kutekelezwa kwa Mkataba wa Paris.

Ripoti hiyo imesema, kiwango cha joto kuanzia mwezi Januari mpaka Septemba mwaka huu kiliongezeka kwa karibu asilimia 1.2 zaidi ya kiwango cha kawaida.
Wakati huohuo, taarifa za awali za mwezi Oktoba zinaonyesha kuwa kiwango cha joto kitaendelea kuwa cha juu mpaka mwishoni mwa mwaka huu, hivyo kupita rekodi ya awali ya joto ya mwaka jana, ambayo ilikuwa ilizidi nyuzi 0.77 juu ya kiwango cha karne ya 20. Ongezeko hilo linasabishwa na tukio la El Nino katika Bahari ya Pasifiki mwaka jana na mwaka huu.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.