Header Ads

Breaking News
recent

Sherehe za 'Diwali' katika mji wa Delhi India zasababisa hali ya hewa kuchafuka.

Wakaazi wa jiji kuu la India, Delhi wameghathabishwa na kile wamesema kuwepo ukungu mkubwa uliosababishwa na fataki nyingi zilizorushwa katika sherehe za Diwali.Mamlaka zilionya uchafuzi wa hewa kutokana na fataki hizo kutumiwa juu ya kiwango kilichowekwa.

 Sherehe za Diwali ni muhimu sana katika imani ya Kihindi na huadhimisha ushindi wa wema dhidi ya ubaya.

Urushaji wa fataki huambatana na sherehe za Diwali na wengi huona hii kama ishara ya utajiri.Familia na kampuni za biashara nchini India hutumia maelfu ya dola kununua fataki ambazo hurushwa usiku wakati wa sherehe hizo.

 Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO} miji 13 kati ya 20 ambayo imechafuliwa zaidi duniani inapatikana India.
Mkali wa filamu na muziki wa kihindi Shahrukh Khan akiwa na mkali mwenzake maarufu kaka mwadada Kajol. Hapo unakumbuka filamu gani walioicheza wakali hawa?

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.