Sayansi na Teknolojia - Kima wanaweza kutengeneza vipande vya mawe vyenye ncha kali kama binadamu wa kale walivyofanya.
Uwezo wa kutengeneza vipande vya mawe vyenye makali na kuvitumia kazini
uliwawezesha binadamu wa kale kuishi vizuri duniani.
Lakini hivi
karibuni wanasayansi waligundua kuwa si binadamu tu wenye uwezo wa
kutengeneza vipande hivi.
Kima aina ya sapajus libidinosus wanaoishi huko Amerika ana uwezo mkubwa wa kutumia mawe. Wanajua kuvunja kokwa kwa mawe, na kuwavutia jike kwa kuwatupia mawe.
Dr.
Tomos Proffitt wa Chuo Kikuu cha Oxford na wenzake walipotafiti kima
hao katika bustani ya taifa ya Serra da Capivara nchini Brazil, waliona
kima hao wanaweza kutengeneza vipande vya mawe ambavyo vinafanana na
vile vilivyotengenezwa na binadamu wa kale.
Kima hao wanapenda kugonga jiwe moja kwa jiwe lingine mara kwa mara, na mara nyingi wanafanikiwa kutengeneza vipande vya mawe.
Ingawa vipande vya mawe
vyenye makali ni vifaa vizuri vya kukatia, lakini kima bado hawajui
namna ya kutumia vipande hivi. Watafiti hawajathibitisha lengo la
vitendo vya kima hao, lakini wameona kuwa baada ya kugonga mawe, kima
hao huyaramba. Dr. Proffitt anafikiri huenda kima hao wanakula unga wa
mawe ili kupata lishe ya silicon au wanakula kuvu kwenye mawe.
Lakini sasa watu wakigundua mabaki ya vipande vya mawe yenye historia
ndefu, hawawezi tena kusema moja kwa moja kama vilitengenezwa na
binadamu wa kale, wanahitaji kufikiria uwezekano kwamba huenda
vilitengenezwa na kima.
Credit: CRI Kiswahili
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA