Header Ads

Breaking News
recent

Miss Tanzania 2016 Diana Edward ameonesha Asili Yetu Tanzania.

Usiku wa Jumamosi Octoba 29, mrembo kutoka Kinondoni, Diana Edward Loy aliziandika headlines pale alipotajwa kuwa ndiye aliyetwaa taji la Miss Tanzania 2016 katika fainali zilizofanyika jijini Mwanza.
 Diana mwenye asili ya kimaasai, kwa muda wote wa ushiriki wa shindano hilo, aliuweka mbele utamaduni wake, kitu ambacho ni nadra kwa Mamiss wengine ambao wengi wao wamekulia mjini.
 
Amekuwa akijihusisha na shughuli za utetezi wa masuala ya kijamii, hasa watu wanaoishi mazingira magumu, pamoja na kampeni za kutokemeza ukeketaji. Wiki moja iliyopita alitoa documentary fupi kuhusu ukeketaji unaofanyika katika jamii yake ya kimasai.
Hongera sana Miss wetu kwa kuwakilisha  utamaduni wa nchi yetu, utamaduni uliosahaulika, ukighubikwa na mila potofu.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.