Header Ads

Breaking News
recent

Maajabu: Mtoto mchanga azaliwa mara mbili!


Mtoto mchanga wa kike kutoka Lewisville, Texas, 'amezaliwa' mara mbili baada ya kutolewa katika kizazi cha mamake kwa dakika 20 ili kufanyiwa upasuaji.

Akiwa miezi minne mja mzito, Margaret Hawkins Boemer aligundua kuwa binti yake, Lynlee Hope, ana uvimbe katika uti wake wa mgongo.

Uvimbe huo unoajulikana kama sacrococcygeal teratoma, ulikuwa unasukuma damu kutoka kwa mtoto huo - jambo lililoongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo kutofanya kazi.
Baby Lynlee alikuwana uzito wa chini ya kilo moja wakati wapasuaji walipomtoa kwenye uzao wa mamake.

Bi Boemer awali alikuwa amebeba mimba ya pacha, lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya kumaliza miezi mitatu ya kwanza. Awali alishauriwa kuitoa mimba hiyo kabla ya madakatari wa wa hospitali ya watoto ya Texas Children's Fetal Center kumpndekezea upasuaji huo wa hatari.

Uzito wa uvimbe huo na ule wa mtoto ulikuwa karibu sawa wakati upasuaji ulipofanywa. Aliarifiwa kuwa mwanawe Lynlee ana asilimia 50 ya kufanikiwa kuishi.

Bi Boemer aliambia CNN: " nikiwa na miezi mitano, uvimbe huo ulikuwa unasitisha moyo wake kufanya kazi, kwahivyo ilikuwa ni uamuzi baina ya kuruhusu uvimbe huo ummalize au kumpa nafasi ya kuishi.
"Ulikuwa uamuzi wa rahisi kwetu: Tulikuwa tunataka kumpa maisha."
'Moyo wake ulisiti kupiga'

Daktari Darrell Cass wa Texas Children's Fetal Centre nimojawapo ya matabibu waliotekeleza upasuaji huo. Amesema uvimbe huo ulikuwa mkubwa, kiasi cha kuhitaji upasuaji mkubwa kuufikia, jambo lililohatarisha maisha ya mtoto huyo.

Moyo wa Lynlee nusra usite kupiga wakati wa upasuaji huo lakini mtaalamu wa moyo alimsaidia kuendelea kuishi wakati uvimbe huo ulipakuwa unatolea, aliongeza.

Madaktari hao baadaye walimrudisha katika uzao wa mamake na kuufunga uzao kwa kuushona.
Bi Boemer alisalia kitandani kwa wiki 12 zilizofuata, na Lynlee alizaliwa kwa mara ya pili mnamo Juni 6.
Source: bbc Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.