Header Ads

Breaking News
recent

Hifadhi kubwa ya viumbe Bahari kujengwa Baharini.

Hivi ni baadhi tu ya vivutio vinavyopatikana chini ya bahari.
Bahari ni eneo kubwa sana la maji lenye viumbe na mimea ya kila aina, huenda wakwetu ungependa kufahamu baadhi ya viumbe na mimea inayopatikana baharini.
Sasa leo nimekutana na hii stori inayoelezea mikakati ya kujenga hifadhi kubwa ya viumbe bahari chini ya bahari.
Miaka ya mazungumzo ya kimataifa imefikia kilele chake kwa makubaliano ya kujenga hifadhi kubwa ndani ya bahari katika maji safi ya Antaktika. 
Nchi ya New zealand na Marekani zimepewa jukumu la kusimamia 1.57 milioni kilomita za mraba za eneo la bahari zinazolindwa katika bahari ya Ross, ambayo ni makazi ya mamilioni ya penguins.
Japo Urusi inazuia mpango huo lakini waziri wa mambo ya nje wa New zealand Murray McCully, amesema kuwa mataifa ishirini na nne yaliyoshiriki mazungumzo hayo yamefikia makubaliano ya kusawazisha ulinzi wa bahari na kuendesha uvuvi na tafiti endelevu za kisayansi.(Story kutoka bbc Swahili)

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.