Header Ads

Breaking News
recent

Bondia Thoma Mashali aaga dunia.

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupigwa na watu wasiojulikana, maeneo ya Kimara Jijini Dar es salaam.

Akithibitisha taarifa hizo, Rais wa Organaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallh “Ostadh” amesema mauti yamemkuta Mashali baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na wasamaria wema maeneo ya Kimara.

Na kwaupande wa Mzee Malifedha Christopher Mashali baba Mzazi wa Thomas Mashali ambaye ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo huko Kimara jijini Dar es Salaam amefunguka na kuelezea kilichomkuta mwanaye. 

Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema Peponi. Amina
Source: EATV

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.