Header Ads

Breaking News
recent

Usain Bolt azidi kufanya vizuri, sasa anyakua medali ya Dhahabu ikiwa ni ya tatu kwake (Rio 2016).

Mwanariadha wa kasi zaidi duniani mzaliwa na Jamaica Usain Bolt amepata dhahabu katika mbio tatu tofauti katika kile kinachojulikana katika kiingereza kama "trible trible" au tatu tatu.

Shindano lake la mwisho lilikuwa la mita 100 kupokezana vijiti mara nne. Alipokea kijiti mwisho katika timu yake na akafululiza kishujaa na kumshinda mpinzani wake wa karibu kutoka Japan, aliyeshinda Marekani na kuchukua Shaba.

Bolt ameshinda dhahabu mara tatu katika Olimpiki zote tatu alizoshiriki ndipo ushindi wake huu ukatambuliwa kama trible trible yaani tatu tatu.

Bolt mwenye umri wa miaka 29, alishinda dhahabu katika mbio za mita 100 na 200 mjini Rio na ndiye mwanariadha wa kwanza kushinda mbio tatu katika mashindano matatu ya olimpiki
Awali timu ya marekani ya wanawake ilishinda mbio sawa na hizo za kupokezana vijiti.

CHANZO: BBC Swahili

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.