Header Ads

Breaking News
recent

Majimbo 25 nchini Marekani yaliyohalalisha matumizi ya bangi kwa matibabu.


Mwaka 2013 nchini Marekani ni asilimia 7 tu ya watu wazima waliokuwa wakitumia bangi.

Lakini kwa mujibu wa utafiti huu uliofanywa na kuchapishwa na Gallup poll, unaonyesha kuwa ndani ya miaka 3 tu, kiwango cha watumiaji wa bangi nchini Marekani kimeongezeka karibia mara mbili yake, ambapo sasa ni asilimia 13.

Japokuwa miaka mitano iliyopita nchini Marekani ilikuwa ni marufuku matumizi ya bangi, lakini sasa kuna baadhi ya majimbo haya nchini humo yameruhusu kisheria matumizi ya bangi kwa matibabu, majimbo hayo ni kama vile:- 
1. Alaska, 2. Arizona 3. California 4. Colorado 5. Connecticut 6.Delaware 7. Hawaii 8. Illinois 9. Maine 10. Maryland 11.Massachusetts 12. Michigan 13. Minnesota 14. Montana 15. Nevada 16. New Hampshire 17. New Jersey 18. New Mexico 19. New York 20. Ohio 21. Oregon 22. Pennsylvania 23. Rhode Island 24. Vermont 25. Washington. 

Na kwa mwaka 2015 pekee watu 9,000 walikamatwa kwa makosa yanayohusiana na bangi, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya Huffington Post.

Nchini Tanzania matumizi ya aina yoyote yele ya bangi, ni kinyume na sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.   

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.