Header Ads

Breaking News
recent

JINSI YA KUITAFUTA GARI YAKO ILIYOPOTEA KWA KUTUMIA SIMU YAKO YA MKONONI.

Hiki ndo kifaa kidogo unachopaswa kukiweka katika gari yako, begi au hata mkoba wako.
Kama wewe ni bingwa wa kusahau unapokuwa umeegesha gari yako katika msongamano wa magari, au gari yako imeibwa, basi wanasayansi wamekurahisishia gharama za kutumia GPS na sasa unaweza kutumia Smartphone tu.

Ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kuweka betri yako ndogo yani (TrackR) maalum kwa kazi hiyo, kisha unapakua app ya bure katika simu yako ya (iphone au Android), kisha unazilink simu na kifaa hicho na baada ya hapo unakiweka kifaa hicho katika gari au begi, mkoba au kwenye kitu chochote unachodhani kinaweza kupotea.


Unachotakiwa  kufanya ni kufungua programu yani (app) kwenye simu yako, bonyeza "kupata kifaa" “find device” icon na itakuambia mahali ambapo TrackR ilipoonekana mara ya mwisho na itakuonesha eneo iliyopo kwa sasa.


Angalia hapo chini jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi....

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.