Header Ads

Breaking News
recent

Jinsi ya kufuga kuku wa mayai hata kama eneo lako ni dogo.

Fursa ya ufugaji kuku imekuwa ni sehemu muhimu sana ya watu wengi waliokwisha igundua katika kujipatia kipato chao. Kila biashara inahitaji ubunifu, ili uweze kuingia katika ushindani wa soko ni lazima uwe mbunifu.
Ufugaji kuku unalipa sana endapo ukiwa na malengo na ubunifu katika uzalishaji, hata kama utaanza na mtaji mdogo wa kuku wachache tu.
Katika maonyesho ya wakulima '88' ya mwaka 2016 jijini Arusha, nilikutana na ubunifu huu wa mabanda ya kufugia kuku wa mayai.

Mabanda haya yametengenezwa kwa jinsi ambayo mfugaji hawezi kupata shida kukusanya mayai, lakini pia kuna tabia ya baadhi ya kuku baada ya kutaga huwa wanadonoa mayai na kuyala, kwa sababu hiyo, mtindo huu wa mabanda utakuwa ni suluhisho kwao.

Pia njia hii ya mabanda ni nzuri kwa wale wafugaji wenye kuku wachache, ambapo mtu anaweza akawa anafuga kuku katika nyumba za kupanga kama unavyojua maeneo huwa ni mafinyu, basi unaweza pia kutumia njia hii.

Ila kwa ushauri na maelezo zaidi kuhusu njia hii ni vyema ukawatembelea wataalamu wa kuku wakushauri zaidi na kukupatia mbinu zaidi za ufugaji kuku.
Tembelea blog hii kila siku ujipatie mbinu nyingi za kimaisha.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.