Header Ads

Breaking News
recent

Computer toleo jipya aina ya Desktop 'Omen X' yenye uwezo mkubwa unaofananishwa na gari aina ya Ferari yazinduliwa.


Computer inayofananishwa na gari aina ya Ferari kiutendaji kazi yatengenezwa. Komputa hii aina ya desktop iliyopewa jina la Omen X, yenye muonekano kama vile spika imetengenezwa na kampuni ya HP.


Kampuni hiyo ya HP imedai kuwa aina hii ya komputa yenye muonekano kama vile spika, imetengenezwa na sehemu tatu za kutolea hewa ili kuruhusu hewa kuzunguka katika komputa hiyo, ambazo zitasaidia kuifanya muda wote kutokupata joto na hivyo kuongeza utendaji kazi mzuri wa komputa hiyo.


Miongoni mwa sifa chache za kompyuta hiyo ya Omen X ni pamoja na ili iweze kufanya kazi ikiwa na vifaa vyote, itakugharimu dola 1,800, ambapo utapa vifaa vyake kama vile Intel Core-i7 processor, 8GB of RAM, a 2TB hard drive supplemented by a 256GB solid-state drive and an AMD Radeon RX 480 graphics card. 

Kompyuta hii pia imetengenezewa USB ports 10! Kompyuta ya kawaida ina kama port 2, 3 au 4 tu, lakini hii ni kiboko ya kompyuta wakwetu.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.