Header Ads

Breaking News
recent

VIDEO YA KUSHANGAZA MTU ALIYEPANDA FUTI 1,500 KUBADILI TAA YA MNARA WA TV.

Huenda ikawa si kawaida kwako kupanda juu umbali mrefu, lakini kwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Daredevil Kevin ni fundi wa kampuni Moja ya TV kusini mwamji wa Dakota nchini Marekani aliyepanda umbali wa futi 1,500 kwenda juu.
Mtu huyo aliyeonekana katika video moja iliyowaacha midomo wazi watu wengi, wakati akipanda umbali wa futi 1,500 katika mnara mmoja ili kubadilisha balb ya taa katika kiunga cha mnara huo.
Kevin ambaye ni mtaalamu anayefanya kazi za minara ya TV aliwashangaza zaidi alipofika mahala akasimama na kujipiga picha mwenyewe yani “Selfie”, na kuendelea na safari yake ya kuelekea kilele cha mnara huo.

Kevin alifanikiwa kufika huko na kubadirisha taa ya mnara huo, na kuacha mishangao mingi katika mtandao wake wa YouTube!

Tazama kipande hiki cha video hii hapo chini…….
 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.