Header Ads

Breaking News
recent

STORY 6 ZA KIPINDI CHA "ZIG ZAG HOT STORY" ZA JANUARY 27 NDANI YA 95.7 IDEA FM.

Zile Story zote za Kipindi cha "ZIG ZAG HOT STORIES"kinachoanza SAA MOJA hadi SAA NNE za usiku kupitia 95.7 IDEA FM RADIO - ARUSHA, Nimekuwekea zote hapa WAKWETU.  


1. Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili wakazi wa Manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kuwanyonga watoto wawili hadi kufa, kisha kuwafukia ndani ya nyumba waliyokuwa wanaishi.

2. Hii ni habari ya kitofauti kabisa, mtoto wa miaka minne anapiga simu namba ya dharura 911 hospitali, kuomba huduma ya ambulance kwa kuwa mama yake alikuwa ameshikwa uchungu anakaribia kujifungua!
 
2. Mtandao wa kijamii wa facebook January 27 ulikuwa hauingiliki ndani ya dakika 40 katika maeneo mengi duniani mapema leo kabla ya huduma zake kurudi.
 

3. Mvulana momoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 9, inasemekana ameurudisha mti katika hali yake ya kuoteshwa ambao ulikuwa umeanguka chini na ulikuwa ukikatwa kuni miaka mitatu iliyopita kwa kuunyanyua peke yake bila kusaidiwa na mtu yoyote .

4. Maelfu ya wanaume nchini Saudia wanajaribu kuwatoa wanawake katika mtandao wa twitter, lakini juhudi hizo zinaonekana kuambulia patupu.
 

5. Mahakama moja nchini Ufaransa imewazuia wazazi kumpatia jina la Nutella mwana wao wa kike, ikisema kuwa jina hilo litamfanya azomwe ama hata kochokozwa.

6. Kampuni moja huko Sweeden ya Erfolg swelle, inasemekana ina uwezo wa kubuni jina la mtoto wako, ambalo linakuwa la kipekee na huwezi kulikuta sehemu nyingine duniani.

Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hichi kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.