Header Ads

Breaking News
recent

NIMEKUWEKEA HAPA STORY ZOTE ZA KIPINDI CHA "ZIG ZAG HOT STORIES" YA JANA JANUARY 23 KUTOKA 95.7 IDEA FM RADIO.

Kama ulikosa wakwetu kusikiliza kipindi kitamu cha ZIG ZAG HOT STORIES kinacho angazia Story Hot Duniani, utazipata 95.7 IDEA FM RADIO ARUSHA kinachoruka Juma Tatu hadi Ijumaa saa Moja jioni hadi saa nne usiku, basi story zilizo husika ziko hapa.....


1. Taarifa sio nzuri kutoka Saudi Arabia, vyombo vikubwa vya habari kama CNN, Sky News na BBC vinaripoti kuhusu msiba wa aliyekuwa Mfalme wa  Saudi Arabia, Abdullah Bin Abdulaziz ambaye amefariki akiwa Hospitalini akipatiwa matibabu. 

2. Mwanamke Vera Jaber amejifungua wakati akiwa kwenye ndege iliyotoka Jordan kuelekea New York, wahudumu wa ndege walitoa msaada kwa mama huyo kujifungua na kundelea na safari hadi walipofika New York ambako mwanamke huyo na mtoto wake walipelekwa Hospitali.
3. Video ya wimbo mpya wa Bebe Cool, Everywhere I Go kutoka kwenye album yake ya,Go Mama Album 2015. Video imeongozwa na God Productions.


4. Ile video ya hip hop iliyokuwa ikisubiliwa sana nchini Uganda hatimae imekwisha dondoka machoni mwa mashabiki wa muziki Afrika Mashariki. Wimbo huo wa video unaokwenda kwa jina la ‘NEW DAY’ ni wa msanii Atlas Da African ft. Lilian Mbabazi, huku Director wa video hiyo akiwa ni Sasha Vybes

5. Mshindi wa Big brother Africa 2014 Idris Sultan ambae anaendeleza matunda ya ushindi wake wa BBA na sasa kajipatia nyumba yake ya kuishi ambayo pamoja na mengine ina sebule mbili na anatarajia kuanza kuishi kwenye nyumba hiyo kuanzia Jumapili January 25 2015.


6. Mratibu wa shirika la kijamii Chiwute alisema, utafiti ulionesha kuwa,wasichana na Wanawake milioni 100 hadi milioni 140 ulimwenguni wanaishi na machungu au madhara yanayotokana na ukeketaji huku waathirika walio wengi wakiwa ni  Kati ya umri wa miaka 15.

7. Mwanamke mwenye umri wa miaka 90 nchini Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi Duniani anayesoma Shule ya msingi.

8. Wema amekanusha vikali kuhusu habari zilizoenea kuwa amempeleka Diamond Platnumz polisi kutokana na deni la milioni 10 alilokuwa akimdai.

Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hiki kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani na WAKWENU CHOTA BOY.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.