Header Ads

Breaking News
recent

NIMEKUWEKEA HAPA HABARI 8 MAARUFU ZA KIPINDI CHA "ZIG ZAG HOT STORY" YA 95.7 IDEA FM - JANUARY 28.

Zile Story zote za Kipindi cha "ZIG ZAG HOT STORIES"kinachoanza SAA MOJA hadi SAA NNE za usiku kupitia 95.7 IDEA FM RADIO - ARUSHA, Nimekuwekea zote hapa WAKWETU.

1. Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, imezipiga marufuku shule binafsi  kuwafukuza au kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani na kusisitiza kuwa shule zote zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

2. Unaambiwa kuwa wageni wengi wanaotembelea bustani ya Cebu Zoo, Ufilipino moja ya vitu ambavyo wanafurahia ni hii ya huduma ya kufanyiwa massage na nyoka aina ya chatu.

3. Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Yamoto Band wameachia audio ya wimbo wao mpya uitwao ‘Tembo’ ikiwa ni siku kadhaa tangu waachie video ya wimbo wao unaofanya vizuri katika soko la muziki nchini “Ntakupwelepweta”.

4. Kwa jamii fulani, wanyama wenye ulemavu usio wakawaida wanakisiwa kuwa na bahati mbaya au laana na kwa wengine ni ishara kuwa jamii hiyo itakumbwa na maafa au janga na mengineyo.

5. Mwanamke mmoja jijini Washington amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kujaribu kuwaua watoto wake watatu kwa kuwakata koromeo ili waache kupiga kelele.

6. Kwa mara ya kwanza mtoto wa msanii wa Marekani maarufu kama Kelly Rowland, Titan kuonekana sura yake hadharani tangu azaliwe, ambapo mara nyingi, Kelly amekuwa akimficha mtoto wake kupigwa picha, hata picha ambazo amekuwa akipost hakuwahi kumuonyesha sura yake.

7. Mshindi huyo wa BBA 2014 Idris Sultan ameanzisha utaratibu wa simu yake kuwa na mtu maalum wa kumuunganisha nae tofauti na awali ambapo alikuwa akipokea mwenyewe. 

8. Mshindi namba mbili wa BBAHotshots 2014, Tayo Faniran
kutoka Nigeria ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Caterpillar ambao amemshirikisha msanii Ebisole.

 Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hichi kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.