Header Ads

Breaking News
recent

KAMA ULIKOSA "ZIG ZAG HOT STORIES" YA JANA JANUARY 22 NDANI YA 95.7 IDEA FM, NIMEKUWEKEA HAPA.

Kama ulikosa wakwetu kusikiliza kipindi kitamu cha ZIG ZAG HOT STORIES kinacho angazia Story Hot Duniani, utazipata 95.7 IDEA FM RADIO ARUSHA kinachoruka Juma Tatu hadi Ijumaa saa Moja jioni hadi saa nne usiku, basi story zilizo husika ziko hapa.....

1. Askari wawili wa kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani wameuawa na majambazi ambao idadi yao haijafahamika. 

2. Spika wa Bunge Anne Makinda amesema sio kazi yake kuwasimamisha wenyeviti wa Kamati za Bunge ambao wanatuhumiwa na ishu ya fedha za Escrow badala yake ni wao wenyewe kujiondoa.

3. Mtandao wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hiyo kupitia programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.


4. Kwa mara ya kumi mfululizo, Real Madrid imeongoza orodha ya vilabu vya soka tajiri zaidi duniani.

5. Madonna akumbwa na maharamia wa mtandao, system ya computer yake imekuwa hacked na mtu kisha akavujisha album ya 13 ya msanii huyo ya ‘Rebel Heart’ na kuuza nyimbo hizo mtandaoni kwa wizi.  

6. Rihanna ameshinda kesi yake dhidi ya duka kubwa la Top shop la nchini Uingereza lililokuwa likiuza T-shirts zenye picha yake.  

7. Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mahmud amepiga marufuku ya matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za Serikali na kusema kuwa, lugha pekee ya mawasiliano itakayotumika katika ofisi hizo ni Kisomali.

Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hiki kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani na WAKWENU CHOTA BOY.

 

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.