Header Ads

Breaking News
recent

HABARI 12 HOT ZA KIPINDI CHA "ZIG ZAG HOT STORY" CHA 95.7 IDEA FM RADIO, JANUARY 26 NIMEKUWEKEA HAPA.

Zile Story zote za Kipindi cha "ZIG ZAG HOT STORIES"kinachoanza SAA MOJA hadi SAA NNE za usiku kupitia 95.7 IDEA FM RADIO - ARUSHA, Nimekuwekea zote hapa WAKWETU.


1. Aliyekuwa waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo alimwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ya kujizulu rasmi kufuatia sakata la Tegeta Escrow lililotikisa nchi kwa muda mrefu.

2. Mshindi wa BBA, Idris Sultan na Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa waliosoma katika shule ya sekondari Mbezi iliyopo Kimara Dar es Salaam, ambapo leo Jan 26 waliwasuprise Wanafunzi wa shule hiyo kwa kuzungumza nao machache juu ya Elimu pamoja na kushare nao picha za kumbukumbu.

3. Rais Kikwete atangaza mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri ambapo kuna waliohamishwa na wapo waliokuwa Manaibu Mawaziri sasa ni Mawaziri.

4. Lupita Nyongo ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi Ulimwenguni, ambapo pia safari hii ameshinda tena katika tuzo za SAG zilizofanyika Los Angeles, Marekani baada ya kushinda  mwigizaji bora akishirikiana na Jared Leto.

5. Mgombea wa chama tawala cha Patriotic Front, Edgar Lungu ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia.

6. Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake mjini Lusaka-Zambia.

7. Utafiti uliofanywa na  kampuni ya SplashData, ya Marekani umeonyesha kuwa password milioni 3.3 zilizotumika mwaka 2014 katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya Magharibi zilivuja.

8. Ripoti moja ya shirika la wahisani  iliotolewa sanjari na mkutano huo wa Davos,ilizua hisia kali baada ya kubashiri kwamba asilimia moja ya matajiri duniani huenda ikamiliki idadi yote ya watu duniani.
 
9. Mike Tyson kajaribu na upande huu, kashirikishwa kwenye wimbo wa Madonna, unaoitwa ‘Iconic’ ambao ni moja ya nyimbo ambazo ziko katika album ya Madonna, Rebel Heart ambayo iliibwa na kuuzwa mtandaoni mwaka 2014 mwishoni na jamaa mmoja raia wa Israel.

10. Katika kesi ya kipekee nchini Misri, daktari mmoja ametiwa mbaroni kwa kosa la kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka 13.

11. Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto leo Jan 26 ameachia rasmi single yake mpya iitwayo Njoo Uichukue amemshirikisha Felly Kano.

12. Vitu vya kumbu kumbu vya aliyekuwa rais wa 16 wa Marekani Abraham Lincoln vimeuzwa katika mnada mjini Dallas nchini Marekani na kupata dola 800,000.


  Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hichi kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani.


 

  

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.