Header Ads

Breaking News
recent

VIDEO YA LADY JAY DEE FT. PROFESSOR JAY - "JOTO HASIRA".

JOTO HASIRA ni bonge la video music kutoka kwa mwanadada Lady Jay Dee akimshirikisha mkongwe wa musiki wa Bongo flava Prof Jay. Video hii kama ilivyokuwa ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki wa muziki nchini, tayari imezinduliwa rasm pale Nyumbani Lounge jijini Dar es salaam.

TIZAMA VIDEO HII


 Haya ndio mashairi ya wimbo wa "Joto hasira"- Lady Jaydee ft. Prof. Jay.
 
Chorus: 
Hili joto hasira, ambaa 
Upepo hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa. 
Foleni njia nzima, ambaa 
Na pesa hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa
VERSE 1: 
Kila siku nimenuna 
Kwanini tunagombana 
Tena tunakosoana, kama tumechanganyikiwa 
Na sioni hata maana 
Ya si kuzinguana 
Yaani kila mtu anajua sana 
Au yote sababu ya?, sababu ya?
Rudia Chorus:
VERSE 2: 
Mazao twalima wote 
Sahani wavuta kwako 
Kama chakula tule wote 
Kwanini chote kije kwako 
Kisu mpini umeshika wewe 
Vitisho kunikata mimi mmmmhh 
Au yote sababu ya? Sababu ya?
Chorus: 
Hili joto hasira, ambaa 
Upepo hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa. 
Foleni njia nzima, ambaa 
Na pesa hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa
Hook: 
Uuuuh, sahau sahau shida 
Oooh ishi ka ziliisha jana 
Say goodbye joto, Rest in Peace Shida 
Knock, knock money
RAP: 
Wenyewe wanasema usawa unakaba 
Na rafiki wa kweli ni mama na baba 
Hawa wengine wala usiwaamini 
Maana binadamu wa sasa wana roho saba 
Watakuwa na wewe kwenye raha 
Na hawatakuwa na wewe kwenye njaa 
Bora nipige misele yangu peke yangu 
Niruke kivyangu na woga niliukataa 
Aaah!! Nabadilika kama saa 
Na Siku hazigandi na sitokataa tamaa 
Wamejaa, usaliti na chuki 
Watu wa karibu wanageuka mamluki 
Jenero nasonga iwe joto au baridi naamini tutashinda 
Kama mbwai iwe mbwai barida 
We make more money rest in peace shida 
Ukinuna unataka tunune wote 
Ukilia unataka tulie wote 
Vita vyako tunapigana wote 
Tukishinda tushinde au bora tufe wote 
Kama kulima kote tumelima wote 
Hata kupanda kote tumepanda wote 
Kupalilia tumepalilia wote 
Aaaargggh !!! nashangaa sasa mbona hatuvuni wote??
Chorus: 
Hili joto hasira, ambaa 
Upepo hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa. 
Foleni njia nzima, ambaa 
Na pesa hakuna 
Ambaa, naruka mwenyewe 
Yelela, yelela, ambaa

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.