Header Ads

Breaking News
recent

PICHA ZA JIJI LA MWANZA KATIKA MUONEKANO TOFAUTI TOFAUTI.

Kwa kiasi kikubwa utaratibu wa usafiri wa dala dala jijini Mwanza ni mzuri, ukipanda gari moja unafika unapokwenda kwamfano kutoka Nyegezi unaunganisha Ilemela Airport.
Hapa ni baadhi ya mitaa ya Mwanza mjini maeeneo ya Chai ya pili.

Hapa ni bandari ya Kamanga ferry, katika jengo hili ndimo mambo yote ya tiketi za kuelekea Bukoba zinakatiwa na kwanyuma yake ndiko meli zinakopakia abiria tayari kwa safari.

Hapa ni nje ya geti la bandari ya Kamanga ferry, wakazi wa eneo hili muda mwingi wako bize na biashara zao.

Hili ni eneo maarufu sana hapa jijini Mwanza, kuna round about yakuvutia sana, watu wengi hutumia kuchukulia picha hapa.

 Hapa ni eneo la kuanikia Samaki katika Soko la Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, likiwa limetapakaa ndege ambao wengine wamesimama juu ya meza za kuanikia Samaki.

 
Hapa ni sehemu muhimu kwaajiri ya kuanikia Samaki katika Soko la Mwaloni Kirumba Mwanza.

Sokoni Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, hapa ni Samaki waliokaushwa kwa jua na tayari wamepangwa sawia kwaajiri ya kusafirishwa sehemu mbali mbali za biashara.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.