Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania
Latest Articles

May 26, 2017

Karibu tena usikilize kipindi cha Hot 112 Radio Show kinachosikika online yani kupitia mitandao mingi hapa Tanzania, kikiwa kimesheheni ubunifu wa kutosha, ambao kwa hakika hutoacha tena kukisikiliza.

Kipindi kimezungumzia matukio makubwa yaliyochukua headlines kuelekea nusu ya mwaka huu wa 2017, ikiwemo ile stori ya matajiri wa dunia, mawaziri, na wasanii.... karibu upakue au usikilize hapo chini, pia tunaomba msaada wako wa kushare kipindi hiki katika account yako ya mitandao ya kijamii.

Tembelea pia ukurasa wetu wa Facebook - HOT 112 RADIO SHOW
Continue reading

May 24, 2017

Hivi umeusikiliza wimbo mpya wa Ben Pol? Anways usijali, hii ni baada ya picha za kushangaza za mkali wa R&B, Ben Pol kusambaa mitandaoni, muimbaji huyo ameachia audio yake mpya ya wimbo ‘Tatu’ akiwa amemshirikisha rapa Darassa....

Unaweza kuusikiliza hapa chini.....
Continue reading

May 17, 2017

Habari zinazozidi kuenea ni kuhusu msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.  

Akiongea na EATV Pili Missana ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha "Back to Life Sober House" amethibitisha kufariki kwa msanii huyo huku akisema alikuwa amelazwa Muhimbili kwa matibabu, kabla ya umauti kumkuta. 

Mungu amlaze mahali pema peponi Dogo Mfaume. Jikumbushe na moja ya kazi yake hapo chini...(Chanzo: EATV)
Continue reading

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo May 17, 2017  Rais mtaafu wa awamu ya nne Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete, ameweka picha tatu zikimuonesha akiwa shambani, na kuweka ujumbe huu.....

"Mapumzikoni kijijini Msoga, tukiendelea na shughuli za kilimo".
Continue reading

Baada ya stori kuzagaa mitandaoni takribani wiki kadhaa ikiambatana na video zilizomuonesha shabiki wa mwanauziki Davido akitishia kujiua endapo hatamuona msanii huyo siku ya kuzaliwa kwake hatimake hit maker wa “if” ameamua kuokoa maisha ya binti huyo.

Shabiki huyo alipost video na huku akisema kama hatamuona Davido ifikapo Agosti 13 basi hana budi kujiua. 

Baada ya video hiyo kusambaa hatimaye Davido amekubali kumuona shabiki yake huyo aliopo Nigeria, katika siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Davido amemuhakikishia shabiki huyo kuwa asiwe na shaka atakuwepo katika siku hiyo muhimu kwake.

Shabiki huyo alisema tangu mwaka 2014 aljaribu kumtumia ujumbe msanii huyo lakini hakufanikiwa kujibiwa hivyo mwaka huu ameamua ni kheri atumie njia hiyo kuonyesha mapenzi ya dhati kwa msanii huyo.

Tazama video hiyo hapo chini..... 
Continue reading

 Chui ni mnyama pori anayepatikana katika hifadhi za hapa nyumbani Tanzania na kwingineko Afrika, mnyama huyu ni kati ya wanayama wanao kula nyama ya wanyama wa aina tofauti na wao.

Hata hivyo tabia ya mnyama huyu imeonekana kuwa tofauti kidogo na wanyama wengine wanaokula nyama.

Chui ameonekana kujali sana chakula chake hivyo hataki bugudha kabisa wakati wa chakula, huenda angekua binadamu wangemuita mchoyo au mbanizi wa vitu vyake.

Unaambiwa chui kupandisha kitoweo chake juu ya mti, kunamsadia kuzuia chakula chake kuibiwa, hii ni kwamujibu wa utafiti uliofanywa mwezi Februari mwaka 2017.

Utafiti uliofanywa na shirika moja lisilokuwa la serikali uligundua kuwa chui katika mbuga ya Sabi Sands nchini Afrika ya kusini huwawinda karibu familia 40 ya wanyama.
Chui hupandisha mtini nusu ya wanyama anaowawinda. Pia hupoteza moja ya mawindo yake kati ya matano kwa wanyama wengine kama fisi, simba na hata chui wa kiume.

Ikiwa chui ataamua kupandisha mtini windo lake na kisha kugundua hakuna mshindani karibu anaweza kuburuza kitoweo kutafuta mti unaofaa ulio karibu.

Mara chui anapokaribia mti hupanda hadi umbali wa mita10 juu kutafuta eneo lililo salama kuning'iniza windo lake.

Hata hivyo wakati mwingine hali huwa ni ya dharura. Kama fisi yuko karibu Chui mara moja anaweza kupanda mti wowote ulio karibu kuzuia chakula chake kuibwa.
Continue reading

Kemikali mbili zinazopatikana katika mimea ya mistuni zinauwezo wa kutengeneza dawa za mpango wa uzazi, ikiwa wanasayansi wangejua wapi wangepata mimea hiyo kwa wingi. 

Kemikali hizo zinapatikana kwenye mizizi ya maua ya dandelion na mmea wa ''thunder god vine'' ambayo umetumika kwa miaka mingi kama dawa za kienyeji.

Sasa watafiti wa Califonia wamesema pia wanaweza kufunga utengenezaji wa mtoto.

Mtaalam wa mbegu za kiume wa Uingereza amesema uzinduzi huo unaweza kuleta njia mpya na ya kudumu ya dawa za mpango wa uzazi kwa wanaume.

Lakini dutu hizo zimepatikana kwa kiwango kidogo kwa mimea lakini gharama ya kupata kemikali hizo kutoka kwa mimea ni ghali sana, kundi moja nchini Marekani limesema.

Katika majaribio, kemikali kwa jina pristimerin na lupeol zilisimamisha ukuaji wa mtoto kwa kuzuia mbegu ya uzazi kupiga mkia wake na kuogelea katika sehemu ya yai la mwanamke. 

Kemikali hizo zilikuwa zimetekeleza majukumu ya '' aina maalum ya mpira ya kondomu'' muandishi wa utafiti huo aliandika kwenye jarida la Proceedings of the National Academy of Sciences.
Kwa namna nyengine waliziba homoni ya kike ya Progesterone inayosababisha mbegu ya uzazi ya mwanamume kuogelea kwa lazima lakini haikuharibu mbegu hiyo.

Haiui mbegu ya uume wala haina madhara yoyote kwa seli za mbegu za kiumeamesema Polina Lishko ,profesa msaidizi wa seli za baolojia kutoka chuo kikuu cha California , Berkeley

Lupeol inapatikana katika mimea kama miembe ,mizizi ya dandelion na Aloe Vera huku pristimerin hutoka kwa mmea wa tripterygium wilfordii unaojulikana pia ''thunder god vine'' na hutumika katika dawa za kienyeji za Uchina.

Watafiti hao wamebaini kwamba kemikali hizo zilifanya kazi kwa kiwango kidogo na hazikuwa na madhara yeyote ikilinganishwa na dawa za mpango wa uzazi zinazotengenezwa ikitumia homoni.

Walihitimisha kwamba kemikali hizo zingeweza kutumika kama za mpango wa dharura wa uzazi kabla na baada ya kujamiana ama dawa za kupanga uzazi maishani kwa kuwekewa dawa hiyo kwenye ngozi. 

Prof Lishko na wenzake wamesema watafanya uchunguzi zaidi kwa nyani ili kubaini jinsi dawa hiyo inavyofanya kazi .
Mbegu za uzazi za nyani ni sawa na za binadamu. Pia wanajaribu kutafuta mbinu za kupata kemikali hizo kwa bei rahisi.
Source:BBC
Continue reading

Vipuli viwili vya almasi, vimevunja rekodi ya dunia kwa kuuzwa kwa kiwango kikubwa zaidi cha pesa, cha takriban dola milioni 58, katika soko la mnada nchini Uswizi.

Vipuli hivyo viko sawa, lakini kimoja kina rangi ya waridi na chengine ni cha buluu.

Viliuzwa tofauti tofauti lakini vikanunuliwa na mnunuzi mmoja.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba vipuli hivyo, vinavyojulikana kama Apollo na Artemis havitakuwa pamoja baada ya kupigwa mnada mjini Geneva.

Viliuzwa tofauti kwa sababu almasi za buluu ni nadra ukilinganisha na zile za rangi ra waridi.

Hata ijapkuwa ziliuzwa tofauti lakini vitasalia kuwa pamoja baada ya kupata mnunuzi mmoja.

Alamasi ya Apollo yenye rangi ya buluu iliuzwa kwa takriban dola milioni 42 huku Artemis yenye rangi ya waridi ikiuzwa kwa dola milioni 15.5.
Na BBC
Continue reading

May 15, 2017

Nyumba ya jirani ilibomolewa na kufanyika mauaji huko nchini Marekani, wauwaji walifanikiwa kutoroka, lakini katika nyumba ya jirani kulikua na kijana mwenye umri wa miaka 18.

Uchunguzi ukafanyika na shuhuda mmoja akajitokeza na kudai kuwa wauwaji ni kijana huyo wa umri wa miaka 18 na wenzake.

Vijana hao walikamatwa na kuhukumiwa kunyongwa, lakini wakiwa bado wako jela yapata miaka 39 - 40 inagundulika kuwa yule kijana mwenye umri wa miaka 18 alihukumiwa kimakosa, hii ni baada ya polisi huko Ohio Marekani kufahamu ukweli na kuamua kuachiliwa huru kijana aliyefungwa akiwa na miaka 18 na sasa akiwa amemaliza miaka 39.

Lakini alipotoka jela alimkuta yule kijana aliyetoa ushuhuda uliomtia hatiani, safari hii akiwa anaumri wa makamo, je kama ni wewe ungechukua maamuzi gani, ili hali umemkuta mtu aliyetoa ushuhuda wa uongo na ukafungwa miaka 39-40?
Continue reading

May 13, 2017

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Zezeta’.

Ambapo Audio ya wimbo huu imeandaliwa na Lizer Classic huku video ikiwa imeongozwa na director, Nic Roux wa South Africa.

Utupie macho hapo chini, na usisahau kudondosha maoni yako....
Continue reading

Harmorapa baada ya kufanya vizuri na wimbowake wa ‘Kiboko ya Mabishoo’ uliotrend sana katika media na kwenye vilongalonga, sasa amejipanga na kuachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nundu’....

Katika wimbo huo amemshirikisha Cpwaa na Ronei. Kuhusu Audio ya wimbo huu imetayarishwa na producer Luffa, huku Video ikiwa imeongozwa na Kwetu Studio.

Sasa tupia macho video hii hapo chini, unaweza pia kutupia hapo chini maoni yako.
Continue reading

May 10, 2017

Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.

Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.

Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.

Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Chanzo: BBC
Continue reading

Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmark kimetengeneza bia mpya kwa kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa kutumia lita 50,000 za mkojo.
Kampuni ya Norrebro Bryghus inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na masalio yoyote ya mkojo wa binadamu.

Pombe hiyo imepewa jina Pisner na imeandaliwa kwa kutumia kimea cha pombe kutoka wka shayiri iliyokuzwa kwa kutumia mkojo huo badala ya mbolea ya kawaida.

Mkojo huo ulikusanywa kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya kaskazini miaka miwili iliyopita 

"Wakati habari kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus.
"Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria tamasha hiyo ya muziki mwaka 2015.,

Lita hizo 50,000 za mkojo zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.

Kutumia kinyesi au mkojo wa binadamu kwa kiwango kikubwa hivyo ni jambo ambalo si la kawaida, baraza la kilimo na chakula nchini Denmark linasema.

Baraza hilo ndilo lililotoa wazo hilo la kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe.

Lakini usishangae, tayari kuna mtambo wenye uwezo wa kubadilisha mkojo moja kwa moja na kuwa bia.

Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja na mbolea ikitumia nguvu za miali ya jua.

Maji hayo, kutoka katika mkojo uliokusanywa kwa siku kumi katika tamasha moja la muziki Ghent kisha yalitumiwa kutengeneza bia.
Chanzo: BBC
Continue reading

May 9, 2017

Orodha hiyo ambayo inaongozwa na msanii wa Nigeria, Akon na nafasi ya pili ikichukuliwa na producer na msanii wa Afrika Kusini, Black Coffee imendaliwa kwa vigezo vya thamani ya endorsement wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo, watazamaji wao kwenye chaneli za YouTube, kutokea kwenye magazeti, kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika mitandao ya kijamii.

1. AKON
Akon anaingia kwenye list hii kutokana na mauzo ya albumu zake akribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100.

2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI
Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black Coffee, ameingia kwenye albumu mpya ya Drake ‘More Life’ ambayo inafanya vizuri sokoni.

3. HUGH MASEKELA
Alizaliwa Witbank, Mashariki mwa Johannesburg, Hugh Masekela ashafanya takriban albumu 43 ambazo zote hizo aliwahi kuperforme na wasanii wakubwa kama Marvin Gaye, Stive Wonder, Miriam Makeba na wengine kibao.

4. DON JAZZY, NIGERIA
Ni msanii pia ni producer kutoka nchini Nigeria ambaye amejibebea umaarufu kutokana na mafanikio makubwa katika game ya muziki Afrika mpaka Marekani ambapo alifanikiwa kuja na label yake ya  Mavins ambayo nayo imebeba vichwa vingi vikubwa vinavyofanya vizuri Afrika, Do Jazzy alianza tasnia ya muziki tangu yuko mdogo kanisani mpaka kufikia hatua hii aliyokuwa nayo sasa. Pia msanii kutoka kwenye label yake ya Mavins, Tiwa Savage alisaini katika label ya Jay Z, Roc Nation.

5. TINASHE, ZIMBABWEAN-AMERICAN
Maarufu na ngoma kama ya “2 On aliyomshirikisha School Boy” pamoja na “How long” ya Davido, Tinashe ni mchanganyiko Mzimbwabwe pamoja na America, vilevile ni mwandishi mzuri wa nyimbo, muimbaji, muigizaji pamoja na dancer. Alishashinda tuzo kibao kupitia wimbo wake wa “2 On”. Tinashe aliingia kwenye listi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutokea katika jarida la Play Boy bila kukaa utupu.

6. JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN
Mzee wa Classic, anajulikana kama Jidenna Theodore Mobisson, mbali na kuwa maarufu katika tasnia ya muziki, Jiddena angekuwa ni moja ya masound Engineer, amejizolea umaarufu na ngoma yake ya Classic Man, Yoga, Long Live Chief na zingine kibao.

7. WIZKID, NIGERIA
Moja ya wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri duniani na kugusa kila mioyo ya wapenda muziki, ameingia kwenye tuzo nyingi kubwa duniani kupitia wimbo wa “One Dance” alioshirikishwa na Drake pamoja na “Come Closer” anayotamba nayo kwa sasa.

8. DAVIDO, NIGERIA
Ni mmoja kati ya wasanii ambao wamepigana sana kufikia hatua ambayo yupo nayo sasa akiwa na ngoma nyingi kali na kutengeneza njia kibao kwa muziki wa Afrika kuchomoza zaidi. Alishapiga kolabo na msanii kutoka Bongo, Diamond platnumz.

9. SARKODIE, GHANA
Alianza kama underground rapper katika tasnia ya muziki wa kiafrika mpaka kufikia hatua ya mghana wa kwanza kushinda tuzo ya BET, maarufu na ngoma “No kissing Baby”, “Pain Killer”.

10. OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE
Albumu 65 zikiwa kwenye tasnia yake ya muziki, katika miaka yake 41 ya muziki, nyimbo zake zimekuwa zikichezwa duniani kote, maarufu zaidi masikioni mwa mashabiki na kibao cha “Neria”
Continue reading